πππππ ππππ πππππ πππππππ πππππππ
ππππ π
Shere bado inabamba kubamba,Dancan ameamua kuspoil majirani kwa chakula kwa sherehe ya ati Dan amenunua gari,lakini maskini wa Mungu,huku nyumbani kwa Mark,there is an intruder,aah! Makosa.
Huku nyumbani,ni Cate mjamzito,Ian mwenye hafeel poa,na Tom, na sasa kuna gaidi ameingia ndani,woi...
Neema wakiwa kwa sherehe,alianza tu kufeel something is weird kiasi,hadi akaambia Mark babe,we better go home,its getting late. Mark akamwambia acha niende basement,nichukue gari nikuje hivi twende, so Mark akatoka akiwa peke yake akaenda basement kuchukua gari lale ndio akuje amchukua Neema waende,makosa ya pili.
On other side, Eddy amekuja na Jojo na Jayden kwake akiambia Jayden sasa huku ndio atakua anakaa na akina Jojo. Jojo alikua jikoni akapika kachai akaletea babake but Eddy hajazoea kuona Jojo jikoni hadi akamuuliza my daughter,kwani unajua kupika chai,last nikiwa na nyinyi kitu ulikua unjua kupika pekee ni mdomo na kelele..Jojo akamwambia yeah Jayden alinifunza..Eddy hapendi kuona Jojo akisifu Jayden,ju hampendi Jayden just because they are from poor,very poor backgroud.
Mark na yeye,kufika tu kwa basement achukue gari,kumbe apart from gaidi mwenye amekuja kwake nyumbani,kuna magaidi wengine walikua wanamngoja huku kwenye wanafanya sherehe.
Gaidi wa nyumbani ashafika ndani,na anatembea pole pole na kuna vitu anatafuta,alikua kwa drawer akapata kuna picha ya Mark an Neema yenye alichora,akaona si hii akaeka kando,akaangalia ingine akapata ya Neema alikua amechorwa akaona si hii pia akaeka kando,kwani huyu na yeye anatafuta nini..ahaaa Chenye anatafuta,alikipata na niwaambie tu ukweli mapema mapema,gaidi...kwanza akiendelea kutafuta,akaangusha glass,makosa,sasa Kate akasikia.
Sikiza, gaidi mwenye ako kwa Mark kwa nyumba si gaidi wa Eddy,huyu ni Amani ama Joseph,ukipenda,sasa makosa ni ameangusha glass na Kate akasikia akamuamsha Tom na Tom kuna gun anakuanga nayo,akajua baaaaaasi,kama kuan wakati yafaa atumie hii gun yake ni wakati huu sasa.
Tom aliamka pole pole kufika akapata ndio Amani anaenda akamwamabia mzee,ni usimame hapo ama nikutoe kichwa na risasi. Amani kuona bunduki,akajua wueh,acha tu atii amri lakini cheki ujinga wa Tom, badala ya kutishia gaidi akiwa mbali alimsongea karibu na kufumba na kufumbua macho, Amani aligeuka,akashika gun ya Tom wakanza kuvurukana na kwa ile harakati,maskini wa Mungu,risasi ilitoka kwa gun,ikampata mbaya mbovu...ilimpata nani? Twende part 2
ππππ π
Mark na yeye kufika kwa parking,alishindwa,hawa ni nani wanamfuata nyuma ikabidi asimame akauliza oya,mnataka nini? Jamaa wakamwambia tunataka kila kitu chenye uko nayo. Huh,Mark aliwaambia hiyo sidhani kama itawezekana lakini walimwambia si ati tunakuomba tunakuitisha. Kufumba na kufumbua macho,Mark alikua ametandikwa vita zingine safi,mbaya makosa. Wueh.
Huku kwake nyumbani nakwo, Kate ashaamka akapata ni Tom pekee yuko hapo chini,Amani ashaenda,kitambo sana na risasi yenye ilipigwa,ilimpata Amani, makosa sana. Kuna damu pale na hiyo damu ni ya Amani.
Tom aliambia Kate yeye ako sawa na damu ni ya yule mwizi ,na ni kweli,Amani kufika nje,ndio anaanza kufeel risasi sasa,wueh! Ni kubaya.
Upande wa pili Mark ashapigwa yuko hali mbaya,na upande huu mtoto wake ambaye ni Amani ashapigwa risasi.
Kumbe Ian, wakati alisikia alichungulia kwa dirisha,akaona yule mwizi,though hakuona sura,but urefu ni wa Jayden but sura ni black,so aliambia akina Kate,huyo mwizi anakaa Jayden but yeye ngozi ni black so si ya Jayden,na kuna tu mtu mmoja mwenye anatoshana na Jayden mwenye ni blacky na huyo mtu ni Nandwa,aah sorry si mimi,huyo mtu ni Amani.
Neema amengoja Mark alete gari anashindwa wait,kwani parking ilihama ama,ikabidi akuje kuona kuna nini Mark hakuji,kufika akapata Mark bado anatandikwa,mbaya mbovu. Wale magaidi kuona Neema,wakahepa but Mark ametandikwa vibaya sana. Walijifanya magaidi ndio Mark asishuku wametumwa.
Huku kwa Eddy,anajisifu sana akiambia Jayde,yeye hufanya vitu kwa utaratibu ju hapendi kufanya vitu cheap cheap. Jayden akakaa akaona hapa hatakaa na fala tu,akaambia Jojo yeye anataka kuenda home its getting late. Wakiwa hapo,Eddy akapigiwa simu akaona ni gaidi wake akatoka kiasi kushika simu.
Eddy aliambiwa washamaliza kazi na wamedeal na yeye venye inafaa.
Mark walikuja wakashtaki police na wakati karao aliuliza Mark kama ako na any enemy maybe,but Mark anajua hana adui akamwambia zii,sina adui hata kidogo lakini Sharon alisema zii,akaambia police,huyu Mark adui wake ni mmoja tu,Eddy bwana wa Neema,na jana kwa party walipigana vibaya sana. Mark hakutaka kusema hii but Sharon akaisema na ikawa recorded.
Sharon alishika msimamo na hata Mark akisema issue yake na Eddy ilikua tu small na wakamaliza,Sharon anasema zii,lazina huyo ni Eddy hadi Dancan akauliza Sharon,mbona unatetea sana Markπ€£π€£π€£π€£Dan hataki kuona bibi yake akitetea Mark.
Wakati huo huo,Mark akapigiwa simu na Kate akamwambia huku nyumbani something has happened. Mark wakatoka teke kuenda nyumbani.
Jayden pia alifikishwa nyumbani na akaambia Jojo wakutane kesho lakini Jayden akishuka,Eddy alimuangalia na macho zingine za wewe kijana nikupate na msichana wangu tena utaona moto but after Jayden ameenda,Jojo kuuliza babake kuhusu Jayden na venye anamuona? Eddy alimwambia Jayden si mbaya viiile but I guess you need someone else mtu kama Amani hivi anakaa poa kuliko huyu Jaydenπ€£π€£π€£
Amani na yeye maskini wa Mungu,lile risasi kwa mkono lilimzidi,damu amevuja mingi sana na yuko kwa barabara.
Eddy na Jojo wamefika nyumbani na wakiwa wamesimama hapo,ndio wakati Neema na Mark wanafika wakiwa wameshikana mikono...Eddy akaona Mark ameumia akamuuliza kwani umepata ajali? Mark akamwambia its nothing.
Sharon pia alikua hapo na akaanza story za mtu kuvamia huku, Eddy kusikia akauliza Neema,yani umeenda out na boyfriend ukaacha mtoto? Sharon akamwambia relax, alimuacha na Kate..Eddy akauliza Kate na yeye ni nani na ju Sharon huwa anadhani Kate ni wife wa Mark, akaambia Eddy haya,kwani humjui,huyo ni wife wa Markπ€£π€£π€£
Eddy alijam akauliza Neema,kwani umeoleka kwa married man? Neema alimwambia I owe you no explanation. Sharon kwa ile harakati,akaropoka akaambia Eddy kwanza wewe tunajua umeenda ukakomboa magaidi waumize Mark,usidhani hatujuiπ€£π€£π€£Jojo kujaribu kuweka mdomo mbele,karibu Sharon akamalize.
Jayden tukimalizia malizia,ashafika nyumbani na anakaa ako soo down sana,hadi Baraza akamuuliza kijana yangu shida ni nini? Jayden akamwambia hakuna kila kitu iko sawa but deep down,Barasa na Salome walifeel there is more to that na wakashuku huenda babake Jojo hajampenda Jayden
End