πππππ ππ πππππ
Team Neema, usisahau kupiga like kabla hujatoka hapa!
ππππππ ππ π
Eddy anaamini kuwa Neema ameolewa na mwanaume mwenye mke, ila Jojo alimwambia baba yake, "Nitakueleza kila kitu, si kama unavyodhani." Eddy akiwa na hofu kuhusu matukio ya hivi majuzi ya uvamizi, alitaka kumuona Ian, lakini Mark akamkataa kwa kusema, "Kwangu huingii." Hapo ndipo mabishano yakaibuka baina ya Eddy na Mark, hadi Babu Jay alipokerwa na tabia ya Eddy na kumrushia ngumi moja kali mdomoni kwa maneno yake machafu. Balaa! Baba mkwe anampiga mkwe wa zamani.
Jojo alijaribu kumweleza babake kuwa Sharon huwa anasumbuliwa na kusahau, na huwa anaishi kwenye dunia yake – si unaona hata sasa anadhani eti ulituma watu wakamshughulikie Mark? Ingawa Eddy ndiye aliyetuma watu kweli, hawezi kukiri hilo waziwazi.
Mark akamjia Tom na kumuuliza, "Sikusema tusitumie bunduki? Vipi kama ungemuua yule mtu?" Kisha akaitisha bunduki hiyo na kusema haitakaa hapo.
Jojo akamwambia babake kuwa yuko shwari na ameondoka.
Lakini kumbe Mark alichapwa vibaya na wale wahuni – maskini! Na hajui kuwa aliyewatuma ni Eddy.
Amani alijitahidi kwa uchovu hadi akaweza kufika kwake na kujitibu mwenyewe – kwa sasa anajisikia nafuu kiasi. Akampigia Eddy simu kumjulia hali, lakini Eddy akambadilishia mada na kumuuliza, "Huyu Jayden, boyfriend wa Jojo, unamfahamu?" Amani akamjibu, "Namjua, mbona?" Eddy akamwambia Jayden amemlaghai Jojo hadi sasa anazungumzia ndoa naye. Akamtaka Amani azungumze na Jojo na kumshawishi aachane na huyo kijana – lakini asiambie Jojo kuwa yeye (Eddy) ndiye aliyemtuma. Anataka Amani amrudishe Jojo kwake, na sio kwa Jayden.
Wacha sasa! Ona Neema anavyomwambia Mark kwa upole, "My love, hata hao majambazi wakija namna gani, bado nakupenda sana, siwezi kuishi bila wewe." Kisha akauliza, "Kuna mtu mmeshakuwa na ugomvi naye hadi akatuma wakushughulikie? Angalia uso wako babe, unakaa kama ugali usioiva!" Mark akamwambia, "Zii, unajua kila kitu changu, sina bifu na yeyote." Neema akasisitiza, "Hata wakikushughulikia vipi, bado ni mimi na wewe mpaka mwisho."
ππππππ ππ π
Kwa upande wa Jayden, baba yake alifika na kumuuliza, "Baba yake Jojo alikataa uhusiano wenu ama vipi?" Jayden akamjibu kuwa kweli, alisema hawezi kuruhusu watoto wake waishi kwenye mazingira kama yale na alikataa kabisa yeye na Jojo waendelee na masomo pamoja. Salome alikuwa nje akisikiliza yote.
Barasa alimhakikishia Jayden kuwa Jojo anampenda sana.
Karen akiwa kwenye shughuli zake, alipokea simu kutoka kwa Eddy, akadhani hatimaye mwanaume wake amerudi. Kumbe! Eddy akamwuliza, "Wewe mwanamke, ulijifanya Neema ukaandika ile barua?" Karen akashangaa na kujiuliza, "Hata handwriting ya Neema siijui! Nilidhani unanitafuta tuwe tena pamoja, kumbe ni ujinga tu!"
Mark alipofika nyumbani, waligundua hakuna chochote kimeibiwa, wakabaki na maswali – nani huyo anayevamia nyumba bila kuiba kitu? Ian akasema, "Alifanana na Amani." Wah! Japokuwa ni mtoto mdogo, hiyo kauli ilizua maswali mengi.
Eddy akapiga simu akasema anakuja kuwaona watoto.
Dancan naye akaingia ofisini tena na kuambiwa kuwa mkopo wake uko tayari. Aliambiwa, "Wewe sasa ndio boss," gari ipo, mafuta yapo na funguo ziko tayari. Aliona dili limekaa safi. Akaachiwa hata ofisi, funguo akapewa, na wale watu wawili wakatoka. Lakini hakuna hata mahali waliandikiana. Jamani, kosa kubwa!
Dana alifurahi sana na akampigia Sharon simu, "Darling! Guess what? Kila kitu kimekubali, kuanzia sasa wewe ni mke wa tajiri!" Dancan hata akamuita Sharon amwone pale alipohamia kama boss.
Eddy alipofika, alikuwa na zawadi kwa Ian. Lakini Ian alikuwa baridi sana kwake hadi Eddy akamwuliza Jojo, "Mbona Ian leo hayuko friendly kama kawaida?" Jojo akamwambia, "Ni kwa sababu jana ulimpigia kelele uncle Mark."
Kuna jambo Mark alihitaji msaada wa polisi, na akampigia Jayden kumpa plate number ya gari – amsaidie kujua ni ya nani na mtu huyo anaishi wapi.
Sharon walipofika ofisini walifurika na furaha – sasa wanajua baba yao ameshaomoka, na hivyo nao wameomoka rasmi. Furaha ilitawala!
Wakati Neema alipomkabidhi Ian kwa baba yake ili waende kuburudika, alimwangalia Eddy machoni akamwuliza, "Niambie ukweli, si wewe uliyehusika na ule uvamizi?" Eddy akageuza macho, Neema akamwambia, "Hapana, niangalie usoni nikikuuliza." Eddy akajibu kwa kizungu kingi, lakini Neema tayari alikuwa na mashaka.
Nimalizie kwa kuwakumbusha – huduma za online bado zinaendelea: SHA, KRA, CV, PP n.k. WhatsApp: 0792181715