ππ„π„πŒπ€ CITIZEN TV πŸπŸ•π“π‡ π€ππ‘πˆπ‹ 2025 π–π‘πˆπ“π“π„π


 ππ„π„πŒπ€ CITIZEN TV πŸπŸ•π“π‡ π€ππ‘πˆπ‹ 2025 π–π‘πˆπ“π“π„π 

𝐏𝐀𝐑𝐓 𝟏 

Mark na Jojo wakifika nyumbani,walipata Neema ashafika already hadi akawauliza yoh,mnatoka wapi? Mark akaambia Neema usijali tulikua na kasmall meeting an Jojo na beef yetu imeisha hadi Jojo akaomba msamaha? Neema akamuuliza Jojo kama ni kweli,Jojo akasema ni kweli but mjue my stand remains...Mark hivyo ndio aliokolea Jojo wasijue alikua kwa trouble.


Mark alimuuliza Neema kuliendaje meeting yake,Neema akamwambia amejitetea na nishampea warning asijaribu kuja between us or else atajua hajui...that was good for Mark as well na tena Mark akamkumbusha Neema akamwambia Barasa alikua ametualika kwake for dinner..si kawaida ya Baraza but Mark alimwambia ni asharudisha wife.


Maelek aliuliza Neema kwenye Ian ako but Neema akamwambia babu yake amemkatalia akasema maybe sisi tuko na maneno yetu kiasi. Babu alichanuka akaona,aha achukue Ian,ndio Mark na Neema wawe na good timeπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚


Kumbe Mark wakijipanga kuenda,Jayden na yeye alikuja kwa Mark washinde na Jojo ndio apee akina Mark na Neema time ya kuongea na wazazi wake na hata Jayden amekuja na movies wawatch ziwakeep busy ju its been a while. Jojo akamwambia ni venye tumekua na tu ish! ish! kiasi, Jayden akamwambia ni kweli,ni venye sometimes nafeel haunipi priority. Jojo hakuambia Jayden walienda an Amani out kikawarambaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚


Dancan na yeye kazi ni paper work tu kwa biashara yake but Sharon anamwambia my dear,hata kama sijui mbona nafeel fishy kiasi kuhusu hii biashara yako but Dan alimwambia usijali bebes,wee tulia nikuonyeshe maajabu. In as much Sharon anataka sana waomoke, anafeel deep down hii biashara si poa. Dan anapiga mahesabu anaona pesa ako nazi hazitoshi so yafaa achukue loan lakini Sharon akamuuliza na security utaeka kama nini ju unajua loan lazima uwe na security? Dan akamwambia so niliona,security niweke hii nyumba yetu. Sharon alishtuka,hadi akaruka juu, "ati what" nyumba yetu uwekelee kama security kwa loan, NEVER EVERπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚


Mark washafika kwa Barasa. Neema na Salome walikua jikoni wakaongea about their issue kiasi za ndoa na za kitambo.


Jojo ana Jayden wako busy wanawatch movie fulani hapo ya Dj Afro,movie ya Alu Arjun akipiga akina Nanabai na RajubaiπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚wanaenjoy sana.


Huku Sharon amewaka anauliza Dan,kwani unaniona mjinga aje? Dan akawaambia sikiza,msiwe na wasiwasi,but incase hii ifail tutauza magari tununue nyumba ingine but Val akamuuliza dad,mbona basi usiweke hayo magari kama security? Dan akasema shida bank haikubali magari kama security. Dan aliwapanga Sharon na Val hadi akaambia Sharon,kubali tu niweke nyumba na nitakung'arisha hadi Neema akikuona anasikia tu poa and just like that,Sharon akafanya one,very big mistake,akakubali,aah! Makosa. wah!


𝐏𝐀𝐑𝐓 𝟐 

Siku iliyofuata,Neema washakuja kazini na Mark huku Neema anaambia Mark, very soon vitu zitakua sawa ju ashapea Eddy stopper hatawai kuwasumbua lakini punde si punde,mwenye alipewa warning alifikaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Yani Eddy tu! Neema akauliza Eddy after kukuambia? You still have guts to come but Eddy akamwambia relax,sijakuja kwa niaba yako,nataka kuongea na Mark man to man...Mark akaona haina shida,twende tuongee.


Eddy alikuja akaomba Mark msamaha kwa kumkosea heshima na Mark akamwmabia haina shida,iam ok,kisha Eddy akaambia Mark,nashukuru sana kwa kusaidia familia yangu but ju nisharudi,kindly I want to take over responsibility lakini Mark akaambia Eddy,unajua hauna akili,mimi sijakuzuia anything na sina uwezo wa kukukataza huo ni uamuzi wa Neema na shida ni hutaki kukubali kuwa Neema hakutaki tena but Eddy alimwambia sikiza,najua Neema sana bado ananipenda na soon atanichose mimi but Mark akamwambia you do whatever you want to do but no at one point umhurt ju nitakutandika vibaya sana..Eddy akamwambia ni sawa,lets see,kati yako na mimi atachose nani and let the battle start.


Eddy alitoka akaenda na akapigia jamaa fulani simu,akamwambia nataka unitafutie wanaume watatu wazuri,nataka wanifunzie mtu adabu. Eddy ameamua kutumia rough way kudeal na Mark sasa,wah! Nikubaya.


On other side, Barasa na Salome penzi limerudi sasa,hadi wanaamka kusaidiana kazi hapo nje. Jayden bado kiburi ako nayo na leo hii anaenda kukutana na babake Jojo,na Salome akamwambia by the way, make sure first impression,it reall matters na hata naeza kukuchagulia nguo poa. Jayden hakukataa akakubali na ina maana kiburi kimeanza kupungua.


Eddy na yeye alienda akatafuta jamaa,gaidi mbaya sana akampea kazi na akamwambia you only have one mission to accomplish,kesho nataka akusikia Mark amevunjwa vunjwa vibaya sana,wueh! Nikubaya sasa...Eddy ameamua kuumiza Mark ndio aachane na Neema,will it work? Tutaona kesho.


NEEMA CITIZEN TV 4 TH APRIL 2025.

 ππ„π„πŒπ€ πŸ’π“π‡ π€ππ‘πˆπ‹ π–π‘πˆπ“π“π„π π„ππˆπ’πŽπƒπ„



𝐏𝐀𝐑𝐓 𝟏 

Kwa kina Mark,story ni Babu Jay na Isabelle venye walikua kwa beach..kumbe hii weekend walienda honeymoon na wakajenjoy sana,si kwa beach,si kupanda ngamia and every enjoyment walikua nayo.


Punde si punde, Sharon akamcall Isabelle,akamuuliza uko wapi? Isabelle kusikia sauti ya Sharon akajua Sharon hayuko sawa akamuuliza shida ni nini? Sharon akamwambia niko sawa,wee fanya chenye unafanya ukirudi uniambie,nataka tuongee....Sharon,anataka kuongea na Isabelle.


Kumbe Eddy na yeye,alikua kwa bossy wa Mark,akamdanganya ati ooh alikua ametravel ju ya biashara na hata Neema ni mke wake. Bossy akamwambia hata ndio anashangaa sana kusikia Neema ako na hubby ju hajawai sikia. Eddy akamwambia so soon nataka kufungua hotel na I guess Neema hatakua anakufanyia kazi tena..Bossy akamwambia na Neema mwenyewe hajaniambia? Eddy akamwambia usijali,atakuamba tu soon.


Kumbe sasaπŸ˜‚πŸ˜‚Amani na Jojo washaanza kuingiana and hii ni baada ya Jojo kumgonga. Jojo akamuuliza ulikua unaenda wapi huku? Amani akamwambia nilikuja kuonana na mzee anaitwa Mark and take some photos za greenhouse although nimeambiwa hapendi mzee wa mapicha picha? Jojo akamwambia Mark namjua,so nitaongea na yeye utakuja kutake photos...Amani akamwambia thats good,si hata unipe number zako just incase uwe free kesho nikuja unipeleke? Jojo akamwambia haina shida, kesho hata nitakua free so nitakupeleka.


Amani already ashaanza kupiga Jojo photos but Jojo akamwambia yoh, don't take my photo sipendi picha kabisa,so Jojo akachukua camera kudelete ile picha lakini kuangalia ile picha akasema nini "this is actually good,so keep it haina haja iwe deleted" πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚


Its around saa tatu ya usiku,Jojo ndii anafika nyumbani,na kumbe amekuja na Eddy..Neema aliona Jojo akismile akamuuliza ni nini? Kumbe washapanga,Eddy akuje na maua kumpea Neema na bila Neema kutarajia,Eddy alikua ashaingia amepiga magoti akimuita my love,take this flowers...Neema akachukua maua na akaambia Eddy, yes this means alot to me na hadi akanusa ile maua akasema wooow this flowers smells nice,hii time yote Mark amenyamaza na amekasirika sana anashindwa mbona Neema achukue maua. Alafu cheki Eddy akaangalia Mark na akasmile na ile macho ya "huyu ni wangu bro"..lakini Neema aliaimbia Eddy sikiza,maua mazuri lakini unasahau kitu moja,to me wewe ni stranger and a nightmare so hutu tupuzi unajaribu kufanya yafaa ujue iam someone's wife to be...Kisha Neema akatupa maua chini na akakanyaga...Mark na yeye akaangalia Eddy and this time round,ni Mark alismile na akaangalia Eddy na ile macho ya "huyu ni wangu brother"πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚


Baraza na yeye akiwa kwake,alibishiwa mlango,kumbe ni Salome na amekuja na bag,na kila kitu chake.


𝐏𝐀𝐑𝐓 𝟐 

Eddy alianza kujam sasa,anauliza Neema mbona unikosee heshima mbele ya mtoto wangu? Neema alimwambia huu ujinga uachane nao,hii blackmail yako sahau kwangu...Mark aliona huyu anapiga kelele akaamka akaambia Eddy,kwangu kelele hutaweza bro..karibu hadi wapigane na Neema akaambia Eddy,wewe chenye nangoja ni divorce tu lakini Eddy alimwambia hakuna divorce hapa,hii yenye unangoja it will take 1yr.


Neema kusikia hivyo,alimcall Richard akamuuliza,si ulisema notification ya divorce takes 1 month? Richard akamwambia yeah but Neema akamuuliza na mbona Eddy ako hapa anasema it wil l take 1yr? Richard akamwambia ni uongo,hakuna kitu kama hiyo,na hakuna kitu ameappeal. So Eddy alikua anadanganya tuπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚


Jayden alikuja akauliza mamake unafanya nini hapa? Salome alimwambia anataka kutulia huku but Jayden alikataa,akamwambia sikiza, sina mama mimi,na wewe si mamangu...Salome alianza tu kulia. Jayden alimwambia mimi mtu najua ni babangu and he is everything to me,so wewe sikujui na sikutambui.


Kwa Mark kulianza kuchemka, Eddy anauliza Neema, so uliona nini kwa huyu mjinga,yani hata huna aibu kufanya hivi mbele ya mtoto,na akianza kuchukua tabia zako za kukaa na mwanaume mwingine?(huyu ni Mark anaitwa mjinga) alafu Jojo pia kanachangia sana but Mark akauliza Eddy, naona unaongea sana,and you are not man enough to confess to your daughter right? Jojo akauliza babake,Mark anamaanisha nini kuconfess kwangu? Eddy akamwambia huyu achana na yeye..Eddy haezi taka Jojo ajue ati alikua na mwanamke mwingine.


Richard na Naomi wake bado wanaletana tu but Richard ashaamua,yeye na Naomi zii...


Salome alikaribshwa na Baraza na hata wakaanza kukula hapo na kumbe Salome ako njaa sana..alikula chakula,mbaya sana. Baraza hana shida na bibi yake,shida ni Jayden.


Salome ashaambia Baraza yeye na Francis washadivorce na Baraza akamuuliza was it by mutual agreement? Salome akamwambia yeah,it was mutual na hata shares zangu niliacha huko.


Jojo kako na mdomo sana. Neema anaambia Jojo watch your mouth lakini Jojo alisema zii,siezi kaa hapa ninyamaze after chenye umefanyia babangu. Mark aliambia Jojo,watch sana mdomo yako lakini Jojo akamwambia wee pia nyamaza,wewe si babangu. Mark akamwambia yeah,you are very lucky iam not your dad ju ile kitu ningekufanyia wewe...Jojo akamwambia nyamaza ndovu,huwezi kuwa ba...b...hata Neema hakungoja Jojo amalizie, alikasukumia kofi moja,mbaya mbovu. Hadi Mark mwenyewe akashtuka. Cate na Tom wako hapo wanajionea kila kitu.


Jojo hana adabu kabisa na kama huwa unawatch Neema na watoto wako,ikifika part ya Jojo,tuma mtoto aende achote maji kwa duka  ama hata aende anunue kiberiti kwa hardware ama umwambia aende butchery aulizie kama wako na panty za 30 bob.


Jayden alitoka,babake akamuuliza unaenda wapi na ni usiku? Jayden akamwambia naenda workout kiasi na usiningoje nitachelewa. Salome aliambia Baraza,our kid really hates me but Baraza akamwambia usijali,its just a matter of time atakua sawa