NEEMA CITIZEN TV 4 TH APRIL 2025.

 ππ„π„πŒπ€ πŸ’π“π‡ π€ππ‘πˆπ‹ π–π‘πˆπ“π“π„π π„ππˆπ’πŽπƒπ„



𝐏𝐀𝐑𝐓 𝟏 

Kwa kina Mark,story ni Babu Jay na Isabelle venye walikua kwa beach..kumbe hii weekend walienda honeymoon na wakajenjoy sana,si kwa beach,si kupanda ngamia and every enjoyment walikua nayo.


Punde si punde, Sharon akamcall Isabelle,akamuuliza uko wapi? Isabelle kusikia sauti ya Sharon akajua Sharon hayuko sawa akamuuliza shida ni nini? Sharon akamwambia niko sawa,wee fanya chenye unafanya ukirudi uniambie,nataka tuongee....Sharon,anataka kuongea na Isabelle.


Kumbe Eddy na yeye,alikua kwa bossy wa Mark,akamdanganya ati ooh alikua ametravel ju ya biashara na hata Neema ni mke wake. Bossy akamwambia hata ndio anashangaa sana kusikia Neema ako na hubby ju hajawai sikia. Eddy akamwambia so soon nataka kufungua hotel na I guess Neema hatakua anakufanyia kazi tena..Bossy akamwambia na Neema mwenyewe hajaniambia? Eddy akamwambia usijali,atakuamba tu soon.


Kumbe sasaπŸ˜‚πŸ˜‚Amani na Jojo washaanza kuingiana and hii ni baada ya Jojo kumgonga. Jojo akamuuliza ulikua unaenda wapi huku? Amani akamwambia nilikuja kuonana na mzee anaitwa Mark and take some photos za greenhouse although nimeambiwa hapendi mzee wa mapicha picha? Jojo akamwambia Mark namjua,so nitaongea na yeye utakuja kutake photos...Amani akamwambia thats good,si hata unipe number zako just incase uwe free kesho nikuja unipeleke? Jojo akamwambia haina shida, kesho hata nitakua free so nitakupeleka.


Amani already ashaanza kupiga Jojo photos but Jojo akamwambia yoh, don't take my photo sipendi picha kabisa,so Jojo akachukua camera kudelete ile picha lakini kuangalia ile picha akasema nini "this is actually good,so keep it haina haja iwe deleted" πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚


Its around saa tatu ya usiku,Jojo ndii anafika nyumbani,na kumbe amekuja na Eddy..Neema aliona Jojo akismile akamuuliza ni nini? Kumbe washapanga,Eddy akuje na maua kumpea Neema na bila Neema kutarajia,Eddy alikua ashaingia amepiga magoti akimuita my love,take this flowers...Neema akachukua maua na akaambia Eddy, yes this means alot to me na hadi akanusa ile maua akasema wooow this flowers smells nice,hii time yote Mark amenyamaza na amekasirika sana anashindwa mbona Neema achukue maua. Alafu cheki Eddy akaangalia Mark na akasmile na ile macho ya "huyu ni wangu bro"..lakini Neema aliaimbia Eddy sikiza,maua mazuri lakini unasahau kitu moja,to me wewe ni stranger and a nightmare so hutu tupuzi unajaribu kufanya yafaa ujue iam someone's wife to be...Kisha Neema akatupa maua chini na akakanyaga...Mark na yeye akaangalia Eddy and this time round,ni Mark alismile na akaangalia Eddy na ile macho ya "huyu ni wangu brother"πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚


Baraza na yeye akiwa kwake,alibishiwa mlango,kumbe ni Salome na amekuja na bag,na kila kitu chake.


𝐏𝐀𝐑𝐓 𝟐 

Eddy alianza kujam sasa,anauliza Neema mbona unikosee heshima mbele ya mtoto wangu? Neema alimwambia huu ujinga uachane nao,hii blackmail yako sahau kwangu...Mark aliona huyu anapiga kelele akaamka akaambia Eddy,kwangu kelele hutaweza bro..karibu hadi wapigane na Neema akaambia Eddy,wewe chenye nangoja ni divorce tu lakini Eddy alimwambia hakuna divorce hapa,hii yenye unangoja it will take 1yr.


Neema kusikia hivyo,alimcall Richard akamuuliza,si ulisema notification ya divorce takes 1 month? Richard akamwambia yeah but Neema akamuuliza na mbona Eddy ako hapa anasema it wil l take 1yr? Richard akamwambia ni uongo,hakuna kitu kama hiyo,na hakuna kitu ameappeal. So Eddy alikua anadanganya tuπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚


Jayden alikuja akauliza mamake unafanya nini hapa? Salome alimwambia anataka kutulia huku but Jayden alikataa,akamwambia sikiza, sina mama mimi,na wewe si mamangu...Salome alianza tu kulia. Jayden alimwambia mimi mtu najua ni babangu and he is everything to me,so wewe sikujui na sikutambui.


Kwa Mark kulianza kuchemka, Eddy anauliza Neema, so uliona nini kwa huyu mjinga,yani hata huna aibu kufanya hivi mbele ya mtoto,na akianza kuchukua tabia zako za kukaa na mwanaume mwingine?(huyu ni Mark anaitwa mjinga) alafu Jojo pia kanachangia sana but Mark akauliza Eddy, naona unaongea sana,and you are not man enough to confess to your daughter right? Jojo akauliza babake,Mark anamaanisha nini kuconfess kwangu? Eddy akamwambia huyu achana na yeye..Eddy haezi taka Jojo ajue ati alikua na mwanamke mwingine.


Richard na Naomi wake bado wanaletana tu but Richard ashaamua,yeye na Naomi zii...


Salome alikaribshwa na Baraza na hata wakaanza kukula hapo na kumbe Salome ako njaa sana..alikula chakula,mbaya sana. Baraza hana shida na bibi yake,shida ni Jayden.


Salome ashaambia Baraza yeye na Francis washadivorce na Baraza akamuuliza was it by mutual agreement? Salome akamwambia yeah,it was mutual na hata shares zangu niliacha huko.


Jojo kako na mdomo sana. Neema anaambia Jojo watch your mouth lakini Jojo alisema zii,siezi kaa hapa ninyamaze after chenye umefanyia babangu. Mark aliambia Jojo,watch sana mdomo yako lakini Jojo akamwambia wee pia nyamaza,wewe si babangu. Mark akamwambia yeah,you are very lucky iam not your dad ju ile kitu ningekufanyia wewe...Jojo akamwambia nyamaza ndovu,huwezi kuwa ba...b...hata Neema hakungoja Jojo amalizie, alikasukumia kofi moja,mbaya mbovu. Hadi Mark mwenyewe akashtuka. Cate na Tom wako hapo wanajionea kila kitu.


Jojo hana adabu kabisa na kama huwa unawatch Neema na watoto wako,ikifika part ya Jojo,tuma mtoto aende achote maji kwa duka  ama hata aende anunue kiberiti kwa hardware ama umwambia aende butchery aulizie kama wako na panty za 30 bob.


Jayden alitoka,babake akamuuliza unaenda wapi na ni usiku? Jayden akamwambia naenda workout kiasi na usiningoje nitachelewa. Salome aliambia Baraza,our kid really hates me but Baraza akamwambia usijali,its just a matter of time atakua sawa

No comments:

Post a Comment